Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU ambaye amewahi kuwa Waziri Mkuu wa Chad ameeleza kusikitishwa na mauaji hayo, huku akitoa mkono wa pole kwa familia ya Deby, serikali na taifa la Chad kwa ujumla kufuatia kifo cha kiongozi huyo.
Naye Volkan Bozkir, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema UN imesikitishwa mno na habari za mauaji ya Deby, na imetuma risala za rambirambi kwa familia ya Deby.
Sambamba na kunyoosha mkono wa pole, Josep Borrell, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amesema pande zote husika nchini Chad zinapaswa kuwa makini na kutanguliza mbele suala la uthabiti wa nchi hiyo na eneo la Sahel kwa ujumla. Kadhalika Charles Michel, Rais wa Baraza la EU amesisitiza kuwa, uthabiti, usalama na mamlaka ya kujitawala Chad zinapaswa kulindwa.
342/